Four Things You Need to Know (Kenyan Swahili Translation)

MAMBO MANNE UNAYOSTAHILI KUJUA

1.      Kwa sababu umevunja sheria ya Mungu, umetenda dhambi kama watu wengine

  • Kila atendaye dhambi amefanya uasi kwa Mungu – soma Waraka wa kwanza wa Yohana 3:4
  • Hakuna mwenye haki hata mmoja – soma Warumi 3:10
  • Wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu – Soma Warumi 3:23


2.      Unastahili kuokolewa kwa dhambi zako

  • Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu wapingao ukweli kwa uovu – soma Warumi 1:18
  • Watu wanawekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu – soma Waebrania 9:27
  • Mshahara wa dhambi ni mauti – soma Warumi 6:23


3.      Hauwezi Kujiokoa wewe mwenyewe

  • Ni kwa nehema pekee kwa njia ya imani mmeokolewa. Wokovu huu hauji kutoka kwa matendo yetu, ili tujivune hila ni kipawa cha Mungu – soma Waefeso 2:8,9
  • Wanadamu hawahesabiwi haki kwa matendo ya sheria – soma Wagalatia 2;16
  • Yesu alisema, “Mimi ndimi njia, ukweli, na uzima, mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi” – soma Injili ya Yohana 14:6

 4.      Ni Yesu Kristo pekee anaye weza kukuokoa kutoka kwa adhabu ya dhambi

  • Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili ya wasio haki ili atulete kwa Mungu – soma Waraka wa Kwanza wa Petro 3:18
  • Kwa maana jinsi hii, Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele – soma Injili ya Yohana 3:16
  • Karama (Kipawa) cha Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu – soma Warumi 6:23
  • Kila amwaminiye Mwana ana uzima wa milele, asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia – soma Injili ya Yohana 3:36

 

MAMBO MANNE NI LAZIMA UFANYE

1.      Ukiri na kuungama dhambi zako kwa Mungu

 Soma Waraka wa Kwanza wa Yohana – 1:9


2.      Acha dhambi zako

Soma Matendo ya Mitume 17:30


3.      Mwamini Kristo Yesu

Soma Matendo ya Mitume 16:31


4.      Mwishie Mungu

Soma Wakorintho wa Kwanza 10:31